Update:

MLIPUKO WA BOMU SHULE YA MSINGI KIHINGA WILAYANI NGARA WAUWA WANAFUNZI 5 NA KUJERUHI 18

Wanafunzi watano wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Kihinga wilayani Ngara mkoani Kagera wamefariki dunia na wengine 18 kujeruhiwa baada ya kulipukiwa na kitu kinachoaminika kuwa bomu.

Mlipuko huo umetokea leo Jumatano Novemba 8,2017 asubuhi wanafunzi hao walipokuwa wakiingia darasani. Mganga Mkuu wa Hospitali ya Misheni Rulenge, Goreti Francis amethibitisha kupokewa miili mitatu na majeruhi 20.

Kati ya majeruhi hao, amesema wawili walifariki wakati wakipatiwa matibabu. Akizungumza kwa simu akiwa eneo la tukio, zaidi ya kilomita 50 kutoka Ngara mjini, diwani wa Kibogora, Adronis Bulindoli amesema wanafunzi waliofariki wana umri kati ya miaka minane na tisa.

Amesema askari polisi kutoka Kituo Kidogo cha Kata ya Bugarama kwa kushirikiana na maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wa kikosi cha kulinda mpaka kilichopo Bugarama wanaendelea na uchunguzi eneo la tukio.
Wataalam wa afya wakitoa huduma kwa majeruhi

Wataalam wa afya wakitoa huduma kwa majeruhi

No comments