Update:

MKURUGENZI WA UFUNDI WA KLABU YA CHELSEA AJIUZULU ……MSTAKABALI WA CONTE MASHAKANI
Mkurugenzi wa ufundi wa klabu ya Chelsea, Michael Emanalo amejiuzulu huku pia mustakabali wa kocha Antonio Conte ukiwa mashakani.

Habari zinaeleza kuwa, kuondoka kwa Emanalo ni pigo kwa mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich kwani amekuwa akimtumia Mnigeria huyo kama mtu muhimu katika bodi ya klabu hiyo.

Emanalo amekuwa ndani ya kablu ya Chelsea kwa miaka 10 huku timu hiyo ikitwaa mataji matatu ya ligi kuu ya England, kombe la FA, kombe la ligi na ligi ya mabingwa.