Update:

MKATABA WA MKOPO WA SH.340 KUUFANYA MKOA WA IRINGA KUWA KITOVU CHA UTALII UKANDA WA KUSINI
Serikali imesaini mkataba wa mkopo nafuu kutoka Benki ya Dunia (WB) wenye thamani ya Sh340 bilioni kwa ajili ya kufungua utalii kwenye mikoa ya Kusini ili nayo ichangie kwenye Pato la Taifa.

Mradi huo unalenga kuufanya mkoa wa Iringa kuwa kitovu cha utalii katika ukanda huo na utaambatana na uboreshaji wa miundombinu, kuvutia utalii na kuibua fursa nyingine za kiuchumi ili wananchi wanufaike na sekta hiyo.

Mkataba huo umesainiwa JANA na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bella Bird na kushuhudiwa pia na Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Gaudence Milanzi.

Akizungumzia mkopo huo, James amesema ukanda wa Kusini una vivutio vingi lakini mchango wake umekuwa mdogo kwa sababu watalii wengi hawaendi kutokana na miundombinu duni na kutotangazwa vya kutosha.

No comments