Update:

MIILI 11 ILIYO PATA AJALI YA NDEGE YAPATIKANA ENEO LA CRETA YA EMPAKAI

Miili 11 ya abiria na rubani wa Ndege ya Shirika la Coastal Aviation iliyoanguka eneo la Creta ya Empakai yapatikana. Ndege hiyo iligonga mlima wa kingo za creta hiyo ilianguka saa saba mchana kutokana na matatizo ya hali ya hewa.
Ilikuwa inatoka Kilimanjaro kwenda Seronera Serengeti ikiwa na abiria 11 na wote wamefariki.
Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Theresia Mahongo amesema zoezi la kutafuta miili limekwenda vizuri. Naibu Mhifadhi wa Ngorongoro, Dk Maurus Msuha amesema wamefanikiwa kuipata miili na kuitoa eneo la ajali kutokana na ushirikiano mkubwa na wenyeji.
Mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo, Lunda Mollel amesema ndege hiyo kabla ya kuanguka ilikuwa inazunguka kutoka eneo la milima zaidi ya dakika 20 hadi baadaye kuanguka baada ya kugonga mlima.
Wakati huo huo, Jeshi la Polisi Mkoani Arusha Mkoani Arusha limeagiza kufanyika uchunguzi kwa ndege ndogo ya aina ya CQ241 ya kampuni ya Coastal iliyo anguka na kusababisha vifo vya watu kumi na moja akiwemo na rubani wa ndege iyo aliye tambulika kwa jina moja la Dewal akiwemo na abiria kumi ambao wanafanyiwa uchunguzi wa utambuzi wa uraiya wao na majina yao .