Update:

KWITEGA AWAASA WAKAZI WA ARUSHA KUZINGATIA LISHE BORA NA KUFANYA MAZOEZI ILI KUKABILIANA NA MAGONJWA

Na Michael Nanyaro


 Ikiwa leo ni siku ya Kisukari duniani imeelezwa kuwa kumekuwepo na ongezekeo kubwa la magonjwa yasiyoambukiza ambapo wito umetolewa kwa wananchi mkoani Arusha kuhakikisha wanazingatia ulaji bora wa vyakula pamoja pia na kushiriki katika mazoezi ili kukabiliana.

 Wito huo kwa wananchi umetolewa na katibu tawala wa mkoa wa Arusha umetolewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha ndg Richard Kwitega katika mahadhimisho hayo ambayo yamefanyika kimkoa,ambapo ameeleza kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la magogonjwa yasiyo ambukiza ambapo sababu kubwa ya magonjwa hayo ni kutokana na wananchi kutofanya mazoezi.
 Hata hivyo licha ya katibu tawala huyo wa mkoa kuzungumza hayo ikiwa ni kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Arusha,Kwa upande wake mganga mkuu wa mkoa wa Arusha dr.Timothy Wonanji anasema asilimia 47 ya vifo vilivyotokea kwa kipindi cha mwezi januari hadi june 2017 vimesababishwa na magonjwa yasiyoambukiza.
Richard Joseph Makao ni katibu wa umoja wa vijana wanaoishi na ugonjwa wa kisukari kanda ya kaskazini anasema changamoto kubwa ni vijana kutokuwa na uelewa juu ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
 Mahadhimisho ya siku ya kisukari Duniani ufanyika November 14 ya kila mwaka ambapo kwa takwimu zilizotolewa zinzeleza kuwa magonjwa yasiyo ambukiza yanaongoza kwa kupoteza maisha ya watu zaidi ya magonjwa ya kuambukiza .

No comments