Update:

Kisa cha Mshambuliaji Aguero wa Argentina kuzimia uwanjani

Image result for aguero argentina Katika hali isiyokuwa ya kawaida jana na iliyoshtua wengi, mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina Sergio Aguero ameanguka na kuzimia wakati wa mapumziko kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Nigeria iliyopigwa jana mjini Krasnodar nchini Urusi.

Taarifa za chama cha soka cha Argentina zinaeleza kuwa hali ya nyota huyo kwa sasa inaendelea vizuri baada ya uchunguzi na matibabu aliyopata katika hospitali iliyopo jirani na uwanja huo.

Katika mechi hiyo Argentina ilikubali kipigo cha magoli 4-2.

Hata hivyo klabu yake ya Manchester City haijatoa neon lolote kuhusu ushiriki wa nyota huyo kwenye mechi ya ligi kuu nchini Uingereza itakapocheza na Leceister mwishoni mwa juma hili.

No comments