Update:

BREAKING NEWS:ALIYE KUWA MUME WA ZAMANI WA IRENE UWOYA NA BEKI WA TIMU YA RAYON SPORTS HAMAD NDIKUMANA AFARIKI DUNIAMsiba mkubwa kwa Taifa la Rwanda! Ndikumana Hamad Katauti amefariki dunia usiku wa kuamukia leo.

Kataut beki wa zamani wa Rayon Sports na mume wa muigizaji maarufu nchini, Irene Uwoya amefariki dunia baada ya kuugua ghafla.

Taarifa kutoka Kigali, Rwanda zinaeleza Kataut alikuwa mazoezini jana asubuhi.

Wakati anapoteza maisha, Kataut alikuwa kocha msaidizi wa kikosi cha Rayon Sports ya Rwanda.

Mara ya mwisho, Kataut aliichezea Stand United ya Shinyanga wakati akitokea Cyprus.


Alikuja nchini mara ya mwisho wakati wa Simba Day Agosti 8, akitua nchini Agosti 7 akiwa na kikosi cha Rayon ambacho kilicheza na Simba na kupoteza kwa bao 1-0.

No comments