Update:

WANANCHI LONGIDO WAFURAHIA KUTUMBULIWA KWA PROFESA MAGHEMBE

Wananchi pamoja na viongozi wa maeneo mbalimbali katika tarafa ya Loliondo wamefurahia kupigwa chini aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe huku wakimsubiri kwa hamu waziri mpya Dk Hamis Kingwangala.

Wamemtaka Dk Kigwangala akutane na wakazi wa eneo hilo ili waweze kumweleza kiini cha mgogoro wa eneo la pori tengefu.

Wakizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana Jumatano katika eneo la Ololosokwan baadhi ya wakazi wa tarafa hiyo walimshauri Dk Kingwangala kutosikiliza majungu bali anapaswa kufika eneo la mgogoro na kupata ukweli.

Diwani wa Kata ya Ololosokwani, Yannick Ndoinyo amesema kwamba Dk Kingwangala anapaswa kukutana na wakazi wa eneo hilo ili waweze kumweleza kiini cha mgogoro unaofukuta mpaka sasa huku akimshauri ajiepushe na wapiga majungu.

No comments