Update:

WANACHAMA WAPYA 239 TAWI LA SINONI JIJINI ARUSHA WAPOKELEWA CCMNA; MICHAEL NANYARO

CHAMA cha Mapinduzi CCM Tawi la Sinoni Jijini Arusha limepokea
wanachama wapya 239 ambao wamejiunga na Chama hicho kutoka vyama
mbalimbali vya kisiasa jambo ambalo limefanya waendelee kujihimarisha
na uchaguzi wa Mwaka 2019-2020.

Tukio hilo limetokea Oktoba 8 kwenye mkutano wa Tawi la Sinoni
ulioitishwa na viongozi wapya waliochaguliwa Mwezi Marchi Mwaka huu
kwa lengo la Mkutano huo,Viongozi kuwashukuru wanachama kwa kuwachagua
Sanjari na kuweka mikakati na kukihimarisha chama kwenye ngazi ya
Tawi na kata .

Mwenyekiti wa Tawi la hilo, Abdalah Yahya Mgongo, alisema kuwa
atafanya kazi za chama mchana na usiku ili kukijenga chama ili kiweze
kuwa na mvuto zaidi ili wananchi wengi waweze kujiunga .

Aliwaeleza wanachama kuwa uongozi mpya unajipanga kuanzisha miradi
kwa kutambua kuwa siasa ya sasa lazima iendane na kuimarisha uchumi
kwenye matawi na hivyo wana Mpango mkakati wa kuzungushia uzio wa
eneo lote la Ccm na vitega Uchumi Vyake .

Aliwataka Viongozi wa Mashina kuhakikisha wanatoa huduma Bora kwa
Wananchi ili kuwavuta wengine kujiunge na chama chao, sambamba na
kufanyika kwa vikao kwa mjibu wa katiba ya Chama ili kuimarisha uhai
wake.

Wakizungumza wakati wa kurejesha kadi za vyama vingine vya kisiasa na
kupokea kadi za Ccm wanachama hao wameeleza kuwa wao walikuwa
wameamua kurejea kutokana na kuvutiwa na utendaji wa mwenyekiti wa
Ccm Taifa Dakta John Magufuli ambaye ndiyo Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania ambapo walisema kuwa hawakushawishiwa na
mwanachama yeyote wa Ccm .

No comments