Update:

TANZANIA YATAJWA KUWA MIONGONI MWA NCHI ZINAZO ONGOZA KWA UZALISHAJI WA ASALI KWA WINGI DUNIANI
Tanzania imetajwa kuwa nchi ya pili duniani kwa kuzalisha tani 38 ELFU za asali kwa mwaka, huku nafasi ya kwanza ikishikiliwa na Ethiopia inayozalisha tani 50 ELFU. Hivyo, Watanzania wamehimizwa kufuga nyuki kwa wingi ili kukuza uchumi kwa kutumia fursa ya upatikanaji asali na nta.

Rais wa chama cha ushirika cha vijana wajasiriamali na wataalamu wa masuala ya nyuki, Philemon Kiemi alisema bidhaa zipatikanazo kutokana na nyuki zimekuwa zikiuzwa kwa bei ya kuanzia Shilingi 500,000/= kwa kilo.

Mtaalamu huyo alisema ushirika huo una hekta 4,000 zilizopo katika Kijiji cha Kisaki mkoani Singida na zinatumika kwa ufugaji wa nyuki sambamba na kuwa kituo cha mafunzo kwa vitendo.

Kuhusu dhana kuwa baadhi ya mikoa imeathiriwa na kemikali za sumu aina ya nikotini kutokana na kilimo cha tumbaku, Kiemi ambaye ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (Sua), alisema ni vigumu kwa nyuki kufyonza sumu kujitengenezea chakula ambacho ni asali.

No comments