Update:

TANROAD BABATI IMEWATAKA WAKAZI WA BABATI KUSIMAMISHA UJENZI UNAOENDELEA NDANI YA MITA 15-30 KUTOKA BARABARANI
Wakala wa barabara Mkoa wa Manyara imewataka wananchi wote waliojenga na kufanya maendelezo mapya ndani ya mita 15 hadi 30 katika maeneo ya barabara wilayani Babati kusimamisha ujenzi na maendelezo hayo mara moja.

Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa TANROADS Mkoa wa Manyara Bashiru Rwesingisa wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Meneja Bashiru amefafanua kuwa licha ya kufanya uhakiki wa majina ya watu wote waliojenga zamani kwa kuwapa notisi na kuchukua takwimu za watu wote waliojenga mita 15 hadi 30 mwaka 2011 bado baadhi ya watu wameendelea kukaidi agizo la kuacha kufanya maendelezo mapya na ujenzi katika maeneo hayo.

Akitolea mfano barabara ya Kiru wilayani humo ambapo ilipanda daraja mwaka 2009 yenye urefu wa kilomita 70 baada ya kukidhi vigezo vya kuunganisha makao makuu ya wilaya na mkoa watu wengi wamevamia na kujenga ndani ya mita 15 hadi 30.