Update:

SEHEMU YA UPELELEZI WA KESI YA MADINI YA ALMASI WAKAMILIKA

UPANDE wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi, inayomkabili Mkurugenzi wa  Tathmini, Archard Alphonce Kalugendo (49) na Mthamini wa Madini ya Almas wa Serikali, Edward Joseph Rweyemamu (50) umeileza mahakama kuwa,  sehemu kubwa ya upelelezi umekamilika bado maeneo machache.
Wakili wa Serikali, Wankyo Simon alimeeleza hayo leo mbele ya Hakimu Hakimu  Mwandamizi, Godfrey Mwambapa wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kesi  hiyo ilipofika kwa ajili ya kutajwa.
Wakili Wankyo amedai  wanakamilisha upelelezi katika sehemu ndogo iliyobakia na  wamewaelekeza polisi kufanya hill na kwamba tarehe ijayo wataieleza mahakama hatua ya upelelezi ilipofikia
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 26, itakapokuja kwa ajili ya kutajwa
Washtakiwa hao wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa  kusababisha hasara ya  dola za Kimarekani 1,118,291.43 sawa na Sh 2,486,397,982.54.
Kalugendo ambaye ni Mkazi wa Kinyerezi na Rweyemamu Mkazi wa Mwananyamala wote ni waajiriwa wa Wizara ya Nishati na  Madini.
Wanadaiwa kati ya Agosti 25 na ,31, mwaka huu, katika maeneo mbalimbali kati ya  Dar es Salaam na Shinyanga, washtakiwa kwa pamoja na kwa vitendo vyao  wakiwa wathamini walioajiliwa na Wizara ya Nishati na Madini  walisababisha hasara ya kiasi hicho cha fedha.

Washtakiwa wa kesi ya uhujumu uchumi, inayomkabili Mkurugenzi wa Tathmini  na mthamini wa  madini ya almasi, Archard
Alphonce Kalugendo (49) na Mthamini wa Madini ya Almas wa Serikali,  Edward Joseph Rweyemamu (50)  wakiingia katika mahakama ya Hakimu Mkazi  kisutu kwaajili ya kusomewa mashtaka yanayo wakabali jijini Dar es Salaam leo.
Na upande wa mashtaka umeileza mahakama kuwa, sehemu kubwa ya  upelelezi umekamilika bado maeneo machache.

No comments