Update:

Polisi ya Las Vegas imewataka wakazi wa mji huo kuwa mbali na maeneo ya Mandalay Bay Casino kutokana na tukio la ufetuaji risasi llilo sababisha vifo vya watu kadhaa


Watu kadhaa wauawa, kujeruhiwa katika ufyatuaji risasi Las Vegas, MarekaniWatu kadhaa wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa katika ufyatuaji risasi uliotokeo katika mji wa Las Vegas nchini Marekani.

Polisi ya Marekani imetangaza kuwa, ufyatuaji risasi huo uliotokea usiku wa kuamkia leo katika tamasha la muziki Mandalay Bay umesababisha vifo vya watu kadhaa na kujeruhi makumi ya wengine.

Polisi ya Las Vegas imewataka wakazi wa mji huo kuwa mbali na maeneo ya Mandalay Bay Casino na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa McCarran. Taarifa ya polisi inasema idadi ya waliouawa au kujeruhwia inafikia watu 20.

Askari usalama wa Marekani wamezingira maeneo muhimu ya mji wa Las Vegas kufuatia mashambulizi hayo. Wahka huko Las Vegas wakati wa shambulizi la ufyatuaji risasi

Kuna habari za kutatanisha kuhusu idadi ya watu waliotekeleza mashambulizi hayo na hadi sasa hakujatolewa taarifa rasmi juu ya nani aliyehusika na idadi halisi ya watu waliouawa.

Maelfu ya raia huuliwa kila mwaka nchini Marekani kutokana na vitendo vya kufyatulia risasi.