Update:

MRISHO GAMBO AWATAKA VIONGOZI WA SHIRILKA LA BIMA KUJALI MASLAHI YA WAFANYAKAZI WAO
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo amewataka viongozi wa shirika la Bima la Taifa kuhakikisha wanaboresha maslahi ya wafanyakazi wa shirika hilo ili waweze kufanya kazi kwa ari na kujiamini.

Gambo alitoa kauli hiyo wakati akifungua kikao cha baraza la wafanyakazi wa shirika hilo kilichofanyika katika ukumbi wa Veta jijini Arusha.

Alisema kwamba ajenda kubwa ambayo inapaswa kutiliwa mkazo katika kikao cha baraza hilo ni pamoja na suala la maboresho ya maslahi ya wafanyakazi wa shirika hilo .

Hata hivyo,Gambo alisema kwamba ushindani wa kibiashara kwa sasa umekuwa mkubwa kutokana na soko huria na hivyo aliwashauri viongozi wa shirika hilo kubadilika na kuendana na kasi ya ushindani huo ikiw ani pamoja na kujikita katika teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA).

No comments