Update:

MOFUGA APATA SULUHU LA MIGOGORO YA MIPAKA KATA YA HYDERERE NA SECHEDA WILAYA YA BABATIMkuu wa Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Chelestino Mofuga ametatua mgogoro wa mpaka baina ya wananchi wa Kata ya Hayderer na Kata ya Secheda Wilayani Babati, uliosababisha machafuko.

Hatua hiyo imetokana na kutokea machafu hivi karibuni ambapo nyumba mbili zilizopo kwenye mpaka wa wilaya hizo zilibomolewa na wananchi waliojichukulia sheria mkononi.

Mofuga akizungumza kwenye eneo hilo, alisema wananchi wa eneo hilo wanapaswa kuishi kwa amani huku wakiendelea kufanya shughuli zao bila kurudia tena tukio hilo.

Alisema yeye na mkuu wa wilaya ya Babati Raymond Mushi, walishawahi kutatua mgogoro huo baada ya kuwatuma wataalamu wa ardhi kutafsiri mipaka ya wilaya hizo mwezi Juni mwaka huu.

No comments