Update:

MAJADILIANO KATI YA WATAALAMU KUTOKA TANZANIA NA KAMPUNI YA BARRICK GOLD MINE YAGEUKA KIVUTIO KWA MATAIFA YA AFRIKA
Rais John Magufuli amesema mafanikio yaliyofikiwa baada ya kuwepo majadiliano kati ya wataalamu wa Tanzania na wale wa kampuni ya Barrick Gold Mine kuhusu biashara ya madini ya dhahabu yameweka rekodi ya aina yake.

Rais amesema hatua inaweza kuzisukuma nchi nyingine za Afrika kuja Tanzania kujifunza namna inavyoweza kujadiliana na wawekezaji wa kigeni na hatimaye kukubaliana.

Amesema kuanzia sasa Tanzania imeweka kiwango kipya kuhusu mikataba ya madini na kwamba kiwango hicho kilichofikiwa na kampuni ya Barrick ndicho kitatumika katika majadiliano na kampuni nyingine.

Rais Magufuli amewataka Watanzania kuendelea kuwa na moyo wa kizalendo akisisitiza jukumu la kuijenga nchi haitafanywa na raia mwingine wa kigeni bali ni wao.

No comments