Update:

MAGUFULI ATOA ONYO KALI KWA WAKURUGENZI WALEVI

Rais John Magufuli, ametoa onyo kwa wakurugenzi wanne wa halmashauri nchini walioanza kujihusisha na matumizi ya kilevi, akiwataka waache mara moja na ikiwezekana waokoke.

Rais Magufuli ambaye hakuwataja wakurugenzi hao, amesema wapo na tayari taarifa zao ameshazipata hivyo waache tabia hizo na badala yake wajikite kuwatumikia wananchi.

Tabia ya ulevi imeonekana kuwa ni dosari kubwa kwa wateule wake, baada ya kutengua uteuzi wa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwangwa mwaka jana kutokana na ulevi.

Rais Magufuli alitengua uteuzi wa Kitwanga baada ya kuingia bungeni kujibu swali linalohusu wizara hiyo akiwa amelewa.

No comments