Update:

LIGI YA TAIFA WANAWAKE KUANZA OCTOBER 26/2017
Ligi ya taifa ya wanawake inatarajiwa kutimua vumbi Novemba 26 mwaka huu ikishirikisha timu 12 zitakazogawanywa kwenye makundi 2.

Mkurugenzi wa ufundi wa shirikisho la soka Tanzania (TFF) Salum Madadi amesema kuwa kila kundi litakuwa na timu 6 zikiwemo 2 zilizopanda msimu huu.

Kabla ligi hiyo kuanza, kutakuwa na semina ya viongozi wa klabu na makamisaa wa michezo.