Update:

LEMA,NASSARI NA MSIGWA KUWAKABIDHI KAZI TAKUKURUWabunge wa Chadema, Joshua Nassari (Arumeru Mashariki), Godbless Lema ( Arusha Mjini) na Mchungaji Peter Msigwa(Iringa Mjini) wamewasilisha Takukuru ushahidi wanaodai unaonyesha wa jinsi madiwani wao walivyonunuliwa kwa kupewa rushwa.

Wabunge wao, wamewasilisha ushahidi huo mchana wa JANA Jumatatu kwenye ofisi za Makao Makuu ya Takukuru zilizopo Upanga Dar es Salaam.

Wabunge hao waliwasili katika ofisi hizo saa nane na dakika 39 mchana na kukutana na waandishi wa habari waliokuwa wakiwasubiri.

Ushahidi huo, wameuwasilisha ikiwa imepita siku moja tangu Lema na Nassari walipofanya mkutano na waandishi wa habari jijini Arusha kueleza jinsi madiwani wao walivyoshawishiwa na kwa rushwa kuihama Chadema.

No comments