Update:

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE AKATAA KUZINDUA DARASA LA SHULE YA MSINGI MKANDIAMBURA WILAYA YA LUSHOTOMkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella amempa siku mbili Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, Kazimbaya Makwega kuhakikisha anawasilisha taarifa ya ujenzi wa darasa la Shule ya Msingi Mkundiambaru.

Hatua hiyo inatokana na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kukataa kulizindua baada ya kubainika limejengwa chini ya kiwango.

Agizo hilo amelitoa leo Jumanne katika Uwanja wa Ndege wa Tanga baada ya kiongozi huyo wa mbio za Mwenge, Amour Hamad Amour kueleza akiwa wilayani Lushoto Septemba 22 aligoma kuzindua darasa hilo kutokana na kuwepo dosari kuu tatu.

Akizungumza wakati akiwaaga viongozi wa Mkoa wa Tanga kuelekea Kusini Pemba leo, Amour amezitaja dosari hizo kuwa ni darasa dogo lisilokidhi vigezo, lina nyufa na limeezekwa kwa mabati ya geji 32 badala ya 28 zinazotakiwa kwenye majengo ya Serikali. Darasa hilo lilipangwa kuzinduliwa wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani Lushoto.

Makwega katika taarifa baada ya Amour kugoma kulizidua jengo hilo alieleza lilijengwa kwa nguvu za wananchi waliotumia Sh7 milioni badala ya Sh11 milioni zilizohitajika.