Update:

KESI YA MAUWAJI INAYO MKABILI MKE WA MAREHEMU ERASTO MSUYA KUSIKILIZWA NOVEMBA 13 MWAKA HUU
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa, jalada la kesi ya mauaji inayomkabili mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita na mfanyabiashara Revocatus Muyella lipo kwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI).

Hayo yameelezwa Octoba 30 na wakili wa Serikali, Patrick Mwita mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya kesi hiyo kuja kwa ajili ya kutajwa,

Kufuatia Maelezo hayo,, Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 13, mwaka huu pia ameusisitiza upande wa Mashtaka wakamilishe mapema upelelezi.

Katika kesi hiyo namba 5 ya mwaka huu, washtakiwa hao wanadaiwa kumuua kwa makusudi Dada wa marehemu bilionea, Erasto Msuya, Aneth Msuya. Tukio hilo, linalodaiwa kufanyika Mei 25, mwaka jana maeneo ya Kibada Kigamboni Jijini Dar es Salaam.

No comments