Update:

KESI YA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA YA MASOGANGE YAPIGWA KALENDA
Video Qeen, Agnes Gerald maarufu kama Masogange akitoka katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mara baada ya kusomewa mastaka yanayomkabiri ya
matumizi ya Dawa za kulevya na kesi yake kupigwa Kalenda mpaka Novemba
14, 2017.

Video Qeen, Agnes Gerald maarufu kama Masogange akizungumza na wakili Rouben Semwanza leo mara baada ya kufika katika mahakama ya hakimu Mkazi kisutu jijini Dar es Salaam leo.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imeipiga kalenda kesi ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili (Video Qeen), Agnes Gerald maarufu kama Masogange hadi Novemba 14 mwaka huu ambapo shahidi wa upande wa utetezi atatoa ushahidi wake.

Mshtakiwa Masogangea alipaswa kuanza kujitetea leo
lakini wakili wa Serikali, Adolf Mkini aliomba kwa Hakimu Mkazi Mkuu,
Wilbard Mashauri kuipangia kesi hiyo tarehe nyingine.

Masogange ataanza kujitetea baada ya mahakama kumkuta na kesi ya kujibu kwa upande wa mashtaka kuleta mashahidi watatu na kuufunga kesi, Masogange pia anatarajia kuita mashahidi watatu.

Masogange anadaiwa kuwa kati ya Februari 7 na 14,2017 katika maeneo yasiyojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin (Diacety Imophine).

Pia anadaiwa kuwa kati ya Februari 7 na 14,2017 alitumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam.

No comments