Update:

DIWANI ALIYE TUMIA KIFAA CHA KUREKODIA WALIYE MSHAWISHI KUJIUZULU AWASILISHA KIFAA HICHO TAKUKURU
Diwani wa Mbuguni wilayani Arumeru mkoani Arusha, Ahimidiwe Rico amewasilisha kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kifaa anachodai alikitumia kuwarekodi waliomshawishi kujiuzulu wadhifa huo.

Uamuzi huo ni baada ya juzi, Oktoba 17,2017 kuhojiwa na maofisa wa Takukuru, leo Oktoba 19,2017 Rico amefika ofisi za taasisi hiyo saa nane mchana kukabidhi kifaa hicho chenye umbo la kalamu anachodai kimetengenezwa nchini Ujerumani.

Akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kukabidhi kifaa hicho, amesema ameitikia wito wa maofisa wa Takukuru waliomtaka akiwasilishe.

Diwani huyo wa Chadema amesema tangu aanze kushawishiwa apokee rushwa kwa lengo la kujiuzulu nafasi yake alirekodi matukio yote na mawasiliano ambayo amekuwa akiwasiliana na baadhi ya viongozi wa Serikali.

No comments