Update:

CCM YASEMA CHANZO CHA UAMUZI WA NYALANDU KUJIUZULU NI HASIRA ZA KUKOSA UWAZIRIChama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida kimesema sababu zilizotolewa na aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu za kuacha ubunge hazina mashiko, isipokuwa kilichomsukuma kufukia uamuzi huo ni hasira za kukosa uwaziri.

Akizungumzia uamuzi wa Nyalandu, mkazi wa Msisi katika Jimbo la Singida Kaskazini, Juma Kindimanda amesema hajawatendea haki wao waliompigia kura kwa kipindi cha takriban miaka 20.

Katika hilo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida, William Mwang’imba amesema kwa jumla wilaya haina shida na Nyalandu na kwa kuwa ameamua kuondoka, basi aende salama.

Tofauti na kauli hizo za CCM, Chadema Mkoa wa Singida imempongeza Nyalandu kwa uamuzi wake, ikisema milango ipo wazi kwa yeye kujiunga na chama hicho. Mwenyekiti wa Chadema mkoani Singida, Shaban Limu amesema kwa mujibu wa katiba ya chama hicho, wanapokea mtu yeyote kutoka kokote kuwa mwanachama.

No comments