Update:

Wivu wa mapenzi chanzo cha mauaji MisungwiMkazi wa Misungwi, Kwilokeja Boniface (35) amemuua mkewe Shija Luchagula (30), kwa kumnyonga kisha na yeye kujinyonga kwa kile kinachodaiwa wivu wa mapenzi. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema leo Jumatatu kuwa tukio hilo lilitokea leo katika kijiji cha Mwiligiligili wilayani Misungwi.

Amesema mwanaume alitoka shambani akakuta tairi nyingi za baiskeli kwenye uwanja wa nyumba yake ndipo ukazuka ugomvi baina yao akimtuhumu mkewe kutokuwa mwaminifu kwenye ndoa yao hivyo alianza kumpiga kwa fimbo kisha kumnyonga mpaka akafariki dunia.

Amesema baada ya kufanya hivyo na yeye alichukua jukumu la kujinyonga kwa kamba ili kukwepa mkono wa sheria. “Kwa sasa polisi wanaendelea na uchunguzi kuhusiana na vifo hivyo na miili ya marehemu tayari imefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazish

No comments