Update:

WATUMISHI WAWILI IDARA YA AFYA SASA WANATAJWA KUREJESHA FEDHA WALIZO KULA KIMYA KIMYA


WATUMISHI wawili wa Idara ya Afya katika Halmashauri ya wilaya ya Igunga,Mkoani Tabora waliokuwa wakikabiliwa na tuhuma za kula shilingi milioni kumi wanatajwa kuzirejesha fedha hizo kimya kimya.

Fedha hizo zilizotolewa na Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto kwa mwaka 2013 na 2014 kwa ajili ya chanjo ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele wamezirejesha fedha hizo kimya kimya.

Waliorejesha fedha hizo ni pamoja na aliyekuwa Mratibu wa chanjo wa wilaya ya Igunga,Mkoani Tabora Bolonja Msange na Msaidizi wake,Novath Bijana.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmaashauri ya wilaya ya Igunga,Bwana Revocatus Kuul ameyasema hayo ofisini kwake alipokuwa akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu fedha zilizorejeshwa na watuhumiwa hao.

Aidha Bwana Kuul amesema katika kipindi cha mwaka 2013 -2014 Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto iliipatia Halmashauri ya wilaya ya Igunga zaidi ya shilingi milioni 150 kwa ajili ya zoezi la chanjo,lakini baada ya ukaguzi ilibainika kuwa shilingi milioni kumi hazikuwa zimefanya kazi iliyokusudiwa.

No comments