Update:

Wakazi wa mji wa Babati wasusia kukabidhiwa mradi wa maji usio kamilika
Wakazi wa kijiji cha Nakwa kilichopo katika Halmashauri ya mji wa Babati Mkoani Manyara wamelalamikia Halmashauri hiyo kwa kuwakabidhi mradi wa maji safi ya kunywa usiokamilika huku mradi huo ukielezwa kugharimu million 800 na kuahidiwa kuhudumia wakazi wote wa kijiji hicho.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti wakazi hao walieleza kuwa ni takribani miezi sita sasa toka wakabidhiwe mradi huo lakini hakuna mafanikio yoyote waliyoyaona . Mradi huo unaoelezwa kuwa chini ya kiwango kwa kuwekwa miundo mbinu dhaifu hasa mabomba ambayo hupasuka ama kupasuliwa na wakulima kwa lengo la umwagiliaji.

Akizungumza kuhusu mradi huo Mkurugenzi wa mji wa Babati Fortunatasi Fwema amekiri kuwepo kwa mapungufu ya mradi huo na kueleza mabomba hayo yapo chini ya kiwango yanapasuka kutokana na kutostahimili presha ya maji hivyo kushindwa kupata maji kama walivyoahidiwa.

No comments