Update:

WAKATI UMEFIKA WA KUNUFAIKA NA RASILIMALI-AFRICANS RISING


Baadhi ya wanafamilia wa Africans Rising wakizungumza na wanahabari baada ya kukamilisha mafunzo na kubadilishana uwezo ya mwezi mmoja yaliyofanyika mkoani Arusha -MS TCDC. Toka kushoto ni M'bongo Ali toka Burundi, Amina Teraz toka Morocco, katikati ni kiongozi wa harakati Mr Muhammed Lamin Saidykhan toka Ghambia ambaye kwa sasa anaishi Senegal, Julie toka Liberia, Mr Omboki Otieno toka Kenya..


Wanaharakati wa masuala ya kijamii, na siasa kutoka nchi kumi za afrika ambao wamekamilisha mafunzo ya takribani mwezi mmoja kuhusu namna sahihi ya kuamsha hisia na kulinda rasilimali , wamesema kuwa WAKATI UMEFIKA WA KILA mwafrika kupigania haki, amani na KUNUFAIKA NA RASILIMALI.
Omboki Otieno ambaye ni mwanaharakati kutoka nchini Kenya amesema kuwa malengo ya harakati hizo ni kuamsha hamasa ya kila mmoja kujiona kama sehemu muhimu katika kulinda rasilimali za Afrika pasina kuwategemea wanasiasa.Omboki amesema kuwa yeye ni mwanafunzi wa misingi ya Azimio la Arusha hivyo anaona fahari kuwa sehemu ya wanaharakati wenye nia ya kufufua hisia za kujali rasilimali za Afrika. Amesema kuwa AFRICANS RISING haipo kwa ajili ya kuvutana na serikali ama wanasiasa bali kumfanya kila mwana Afrika kujioni kuwa muhimu kwa rasilimali.

Mbongo Ali ambaye ni mwanaharakati kutoka Burundi amesema kuwa suala la demokrasia bado limekua ni changamoto ambayo inakwamisha maendeleo ya kweli lakini jambo hilo halitamalizwa kwa kulalamika bali kila mwana Afrika kuamka na kuchukua hatua ikiwemo kukemea wazi wazi.

Miongoni mwa nchi zinazo shiriki katika maadhimisho hayo pamoja na kujifunza mambo mabalimbali kwa ajili ya kutetea haki,amani na utu wa mwafrika ni nchi ya Senegal,Kenya,Morocco,Congo,Liberia,Somalia,Burundi,Uganda,Benin na Tanzania.
No comments