Update:

Viziwi waomba kushirikishwa kwenye mipango ya maendeleo


Mwenyekiti wa chama cha viziwi nchini Nidrosy mlau ameishauri serikali kuangalia upya sera ya ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu wa kusikia kwenye mipango ya maendeleo ili kunid hilo liweze kushiriki kikamilifu kwenye kukuza uchumi wa taifa.

 
Bwana mlau anatoa rai hiyo  jijini Arusha  wakati wa uzinduzi  rasmi wa mradi wa ushirikishwaji wa watu wa kundi hilo kwenye  mipango mbalimbali ya maendeleo unaofadhiliwa na asasi ya  foundation for civil society bwana Mlau ..Nidsory Mlau-Mwenyekiti chama cha viziwi taifa. 

Akizungumza walemavu waliohudhuria  uzinduzi huo mwakilishi wa mkuu wa wilaya ya arusha Felician Mtehengerwa anasema tayari yapo mambo yanayotekelezwa kupitia sera ya taifa ya watu wenye ulemavu likiwemo la kila halmashauri ya wilaya kutenga asilimia mbili ya mapato yake kusaidia watu wenye ulemavu….Felician Mtehengerwa-mwakilishi wa mkuu wa wilaya arusha.
 
Changamoto nyingine inayotajwa  kuwatatiza  watoto wenye ulemavu  ni uhaba  wa miundombinu rafiki ya ufundishaji kwenye shule zenye vitengo maalum .wazazi wenye watoto wenye ulemavu wakaiomba serikali kufanya maboresho na kupanua wigo wa utoaji elimu…anna julius na john abraham-wazazi wa watoto wenye ulemavu.


No comments