UTATA,SIMANZI NA MAJONZI IMEWAKABILI WAKAZI WA ARUSHA BAADA YA MIILI YA WATOTO WANAO SADIKIKA KUWA WALITEKWA KUKUTWA IMEKUFA

Wananchi jijini
hapa wamekumbwa na hofu baada ya jana jioni kukutwa kwa miili katika eneo la Olkerian Kata ya Olasiti Jijini Arusha
ambayo iliibiwa hisia kuwa huenda ya watoto waliotekwa ambao walikuwa
hawajapatikana.
Watoto hao;
Moureen David (6) anayesoma darasa la kwanza katika Shule ya Msingi
Lucky Vincent na Ikram Salim (3), wakazi wa Kata ya Olasiti jijini Arusha
wanadaiwa kutekwa huku polisi mkoani Geita wakimshikilia Samson Petro anayedaiwa kuwa mtuhumiwa mkuu .
Wakizungumza jana
huku wakiwa wamekusanyika katika eneo la Olasiti Mtaa wa Olkerian katika Kata
ya Olasiti; baadhi ya wananchi walisema
kuwa wanasubiri taarifa ya polisi ambao ndio waliosimamia utoaji wa miili hiyo
ili ifanyiwe uchunguzi na kubainika kuwa ni ya nani.
Awali , Mwenyekiti wa Mtaa wa Olkerian katika Kata ya
Olasiti walikotekwa watoto hao, Daudi Safari amesema wana imani watoto hao
watapatikana kutokana na kazi inayofanywa na polisi na wananchi.
No comments