Update:

POLISI YATUMIA MABOMU KUVUNJA MKUSANYIKO WA WAFANYAKAZI WA KAMPUNI YA KICHINA WILAYANI SIHA
Jeshi la polisi wilayani Siha mkoani Kilimanjaro liliwatawanya kwa mabomu ya machozi, wafanyakazi wa zamani ya kampuni ya Geo Engineering ya China, wanaodaiwa kuhamasisha wanaoendelea na kazi wagome.

Tukio hilo la kutawanywa kwa mabomu ya machozi kwa wafanyakazi hao, lilitokea saa MOJA asubuhi baada ya wafanyakazi hao wa zamani wanaodai kutolipwa mafao yao, kukusanyika nje ya eneo la mradi wakitaka kuungwa mkono na wenzao.

Inadaiwa kuwa wafanyakazi hao walifanikiwa kuwashawishi baadhi ya wanaoendelea na kazi ili nao wagome kama njia mojawapo ya kushinikiza uongozi wa kampuni hiyo kuwalipa stahiki zao baada ya kuachishwa kazi.

Akizungumzuia suala hilo, Mkuu wa Wilaya ya Siha, Onesmo Buswelu alisema waliofanya mgomo huo ni kikundi cha watu wachache wanaojiita ni viongozi wa wafanyakazi ambao ndio waliosambaza barua za kuhamasisha mgomo huo.

No comments