Update:

MWENGE WA UHURU KUTUMIA BILIONI TANO KUZINDUA MIRADI 9 JIJINI ARUSHAMWENGE wa uhuru unatarajia kuweka mawe ya msingi, na kuzindua miradi tisa yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni tano katika maeneo mbalimbali ya jiji la Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa mkurugenzi wa jiji la arusha,Bw.Athuman Kihamia,alisema kuwa mwenge huo utapokelewa jijini hapa septemba 5,ukitokea Wilayani arumeru Mkoani hapa.

Kihamia alisema kuwa mwenge wa uhuru utapokelewa katika eneo la Chekereni,ambapo utazindua kambuni ya kisasa ya nyama,utatembelea kikundi cha akina mama na vijana cha Engutoto,miradi mbalimbali ya barabara,miradi ya maji Lemara na kikundi cha akina mama Eserian ambapo mkesha utafanyika katika kata ya Sombetini jijini hapa.

Ametoa wito kwa madiwani hao na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa hususani vya upinzani kuachana na kuwahamasisha wananchi na wafuasi wa vyama vyao kususia shughuli za mwenge na badala yake wawahamasishe wajitokeze kwa wingi.

No comments