Update:

Migogoro ya familia yapelekea jamaa kumuua mkewe na kujeruhi wakwe zake

Jeshi la polisi Mkoani Kilimanjaro limethibitisha tukio la mwanaume kumuua mke wake na kuwajeruhi vibaya wakwe zake huko Wilayani Same Mkoani kilimanjaro ambapo tukio hilo limetokana na migogoro ya kifamilia

Akizungumza na waandishi wa blog hii Kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro Hamis Issa amesema Mwanaume aliachana na Mke wake na mwanamke akaamua kurudi kwa wazazi wake mwanaume akamfuata huko na kisha ugomvi ukazuka akaanza kumpiga mkewe na pamoja na wakwe zake na mpaka kupelekea kifo na kuwajeruhi vibaya wazazi Jeshi hilo linamshikilia mtuumiwa huyo kwa mahojiano zaidi 

Aidha kamanda Hamis ametoa rai kwa wanandoa kuwa wajuwe jinsi ya kutatua tatizo lakifamilia sio kuchukua uamuzi  unaopelekea kutenda kosa na likakugarimu baadae uamuzi wa kupiga mwanamke sio mzuri lazima mkae chini kisha muyamalize

kwa taarifa zaidi utazipata kupitia  Sunrise Radio Arusha  

No comments