Update:

MC Pilipili aruhusiwa Hospitali

Emmanuel Mathias maarufu kwa jina MC Pilipili ameruhusiwa kutoka hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza baada ya kulazwa kwa takriban siku nane. Daktari bingwa wa upasuaji hospitalini hapo,Hans Klaud ambaye pia amekuwa akimpa huduma za kitabibu anasema wameridhishwa na hali ya mgonjwa wao kabla ya kumruhusu.

 Mkali huyo wa kuvunja mbavu alilazwa Bugando mara baada ya kupata ajali iliyohusisha gari lake binafsi Septemba 12 mwaka huu mkoani Shinyanga. Hata hivyo, MC Pilipili amepata majeraha ya kifua, kichwa na kiunoni hali iliowalazimu wataalam wa afya Bugando kumfanyia vipimo vya kina ikiwemo CT Scan na Chest-Scan ili kubaini kama alipata madhara 'kwa ndani'. Vipimo hivyo vilirejesha majibu chanya kwamba MC Pilipili hakuumia kwa ndani bali alipata majeraha tu, yaani external injuries.

No comments