Update:

Masumbwi: Rio Ferdinand kaingia kwenye masumbwiBeki wa kati wa zamani wa Manchester United, Rio Ferdinand ametangaza rasmi kuingia kwenye mchezo wa ngumi na tayari ameshaanza mazoezi kwaajili ya kuingia ulingoni.

Muingereza huyo amethibitisha atafanya masumbwi kama bondia rasmi na sio kwasababu tu ya kufurahisha nafsi yake. Ferdinand akiwa Manchester United alifanikiwa kutwaa ubingwa wa England mara 6 pamoja na UEFA mara moja na hivi sasa anafanya kazi kama mchambuzi wa soka kwenye runinga.