Update:

Mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Marekani nchini Somalia yamefanikisha kuwaua wapiganaji watatu wa Al Shabaab nchini humo

Mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Marekani nchini Somalia yamefanikisha kuwaua wapiganaji watatu wa Al Shabaab nchini humo.
Kwa mujibu wa habari zilizotolewa na AFRICOM ni kwamba mashambulizi hayo yamefanyika katika mkoa wa Bay nchini Somalia.
Ripoti zinaonyesha kuwa mashambulizi hayo yamefanywa na Marekani ikishirikiana na serikali ya Somalia pamoja na AMISOM.
AFRICOM imesema kuwa majeshi ya Marekani yatazidi kuisaidia Somalia katika kupambana na ugaidi wa Al Shabaab nchini humo.
Al Shaabab ilitambuliwa na Marekani kama kundi la kigaidi toka mwaka 2008.