Update:

Kutoa Khaligharaph Jones, Roma na Stamina waondoka Nairobi na kolabo 3

Muunganiko wa wasanii wawili Roma na Stamina, Rostam umefanya kolabo tatu na wasanii kutoka Nairobi nchini Kenya.Hapo jana wasanii hao kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii waliweka wazi kufanya kolabo na rapper Khaligharaph Jones lakini imeeleza kuna wengine wawili.

Rapper Stamina akizungumza na XXL ya Clouds Fm amesema walipoenda katika nchi hiyo walikuta kazi yao imekuwa kubwa kuliko walivyodhani hapo awali.

“Tumekuta imekuwa kubwa hatukutegemea mapokezi yamekuwa makubwa kwa hiyo tunamshukuru Mwenyenzi Mungu tumefanya media tour kuanzia Mombasa na Nairobi,” amesema Stamina.

“Tumefanya kolabo tatu na wasanii wa Nairobi na video moja, kolabo na Khaligharaph hiyo ndio ipo official, hizo mbili nyingine tumeziweka kama exclusive,” ameongeza.

Roma na Stamina ‘Rostam’ kwa sasa wanafanya vizuri na ngoma yao mpya ‘Hivi Ama Vile’ na mwaka huu wanatarajia kutoa albamu.

No comments