Update:

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA, DKT JUMA MALEWA APOKEA MISAADA YA KIBINADAMU YA WAFUNGWA, MKOANI KILIMANJARO


Mwenyekiti wa New Life In Christ Mkoani Kilimanjaro, Bi. Elly Makyao (kulia) akikabidhi misaada ya kibinadamu ya Wafungwa waliopo Magerezani nchini kwa Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, Dkt. Juma Malewa. Hafla fupi ya Makabidhiano ya Misaada hiyo imefanyika leo Septemba 08, 2017 katika Viwanja vya Gereza Kuu Karanga – Moshi, Mkoani Kilimanjaro.

Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, Dkt. Juma Malewa akitoa hotuba fupi wakati wa hafla ya kupokea misaada ya kibinadamu kwa Wafungwa waliopo Magerezani iliyotolewa na Asasi ya "New Life In Christ" leo Septemba 08, 2017 katika Viwanja vya Gereza Kuu Karanga - Moshi, Mkoani Kilimanjaro.

Mkurugenzi wa Doricas Aide International - Tawi la Tanzania, Bi. Lilian Urasa akitoa maelezo mafupi namna Shirika linavyoshirikiana na Serikali katika Nyanja mbalimbali hapa nchini.

Aina mbalimbali ya misaada ya kibinadamu iliyotolewa kwa Wafungwa waliopo Magerezani nchini na Asasi ya "New Life In Christ". Hafla ya Makabidhiano ya misaada hiyo imefanyika leo Septemba 08, 2017 katika Viwanja vya Gereza Kuu Karanga, Moshi ambapo Mgeni rasmi alikuwa ni Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa.

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa akiwakabidhi cheti cha shukrani Viongozi wa Asasi ya "New Life In Christ" kwa kutambua mchango wao kwa niaba ya Jeshi la Magereza Tanzania na Serikali kwa ujumla.

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa akimsukuma askari ambaye ameketi kwenye Baiskeli Maalum ya kubebea wagonjwa wasiojiweza ambayo ni miogoni mwa vifaa mbalimbali vilivyotolewa kama msaada kwa Jeshi la Magereza na Asasi ya "New Life In Christ"(kushoto) ni Mkurugenzi wa Doricas Aide International anayeshughulikia Miradi ya Afya katika nchi za Africa, Bi. Mirjam Verwij.

Baadhi ya Wakuu wa Magereza waliohudhuria hafla hiyo wakifuatilia kwa umakini hafla ya tukio hilo kama inavyoonekana katika picha.

Mkuu wa Magereza Mkoani Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Julius Sangu’udi(wa kwanza kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Magereza Mkoa Tanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, John Masunga na Mkuu wa Magereza Mkoani Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Ramadhani Nyamka kama inavyoonekana katika picha.

Wafungwa wa Kike wa Gereza Kuu Karanga, moshi wakionesha mikate na skonsi zinazotengenezwa na wafungwa wa Kike katika gereza hilo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa programu mbalimbali za urekebishaji magerezani.

Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, Dkt. Juma Malewa(katikati) akiwa katika picha ya pamoja Askari wa Magereza Mkoani Kilimanjaro(waliosimama) pamoja na Viongozi Wawakilishi wa Asasi ya "New Life In Christ" mara baada ya kupokea misaada ya kibinadamu ya Wafungwa waliopo Magerezani nchini (wa kwanza kushoto) ni Mwenyekiti wa New Life In Christ Mkoani Kilimanjaro, Bi. Elly Makyao(wa pili kushoto) ni Mratibu wa Huduma za Magereza toka Asasi ya "New Life In Christ", Bw. Charles Shang'aa (wa pili kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Arusha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Khamis Nkubasi( wa tatu kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Hassan Mkwiche (Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

No comments