Update:

Kamati ya Nidhamu TCRA yatembelea Sunrise radio na kuzungumza na Uongozi

Vyombo vya Habari nchini vimekumbushwa kuandaa na kusimamia maudhui yanayo jenga jamii badala ya kukumbatia tamaduni za nje ambayo kwa kiasi kikubwa yana bomoa uzalendo nidhamu na tamaduni za nchi 
Hayo yamesemwa na mmoja wa maofisa kutoka katika kamati ya nizamu TCRA wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Bi. Vallerie Msoka walipo tembelea makao makuu ya Sunrise Radio na kuzungumza na wakuu wa vitengo mbalimbali akiwemo mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho Ndg. Dionis Moyo