Update:

HUDUMA YA KWANZA KWA MTU MWENYE PRESHA YA KUSHUKA.

By Dr Emanuel Mabisi

Presha ya kushuka au shinikizo la chini la damu (hypotension) hali hii inatokea pale msukumo wa damu unapakua mdogo na dhaifu, halo ambayo husababisha viungo muhimu katika mwili (major organs) kushindwa kupokea kiasi cha damu na oksijeni kinacho jitosha

Sababu zinazopelekea presha kushuka (shinikizo la chini la damu)
-Mshtuko
-Kukata tamaa
-Kuwa na mawazo mengine yaliyopitiliza
-kula mlo usio kamili ,(vitamini, proritini, na ukosefu wa madini)
-Kuwa na upungufu wa maji mwilini
Dalili anazoonyesha mtu mwenye presha ya kushuka
-kuishiwa nguvu ghafla
-kuona ukungu
-Mdomo kukauka
-Kizungu zungu
-Kupoteza fahamu

Jinsi ya kutoka huduma ya kwanza kwa mtu mwenye presha ya kushuka
-Kama mtu huyo ataanza kujisilkia kizunguzungu, muweke akae katika kitu au mlaze chini
-Mnyanyue kichwa chake kama umemlaza chini , kwa kumuwekea mto (pillow) chini ya kichwa chake
-Andaa maji ya vugu vugu kiasi cha Lita moja na changanya na chumvi vijiko viwili vya chakula, kisha mnyweshe taratibu na kwa umakini maji hayo kuepuka majeruhi kupaliwa
-Kuwa makini unapomuinua kutoka chini au sehemu aliyokuwa amekaa, kwasababu muinuko wa ghafla unaweza kuzidisha kupunguza msukumo wa damu
-Hali hii ikidumu kwa muda mfunge mgonjwa katika mguu wake wa mbali, nchi tano kutoka chini ya goti kwakutumia lastiki au mpira unao vutika ili damu isiende chini ya miguu na kufanya damu ibakie hasa sehemu ya juu ya mwili
- Kama unaweza kupata maziwa ya mtindi, mpatie mgonjwa kwakuwa huwa yanasaidia kwa wagonjwa kwenye presha ya kushuka
-Muwahishe mgonjwa hospitali haraka ili aweze kupatiwa matibabu
kumbuka
-Punguza kunywa vinywaji vyenye vileo kama (alcohol au kafein)
-Jitahidi kula matunda na mboga mboga katika mlo wako
-Jitahidi kunywa maji mengine ili kuepuka ukosefu wa maji
-Usipende kunyanyua vitu vizito sana
-Jitahidi kufanya mazoezi ya viungo mara kwa mar