Update:

FIFA kuipiga tafu Kombe la Challenge kwa wanawake (CECAFA)


Bodi ya chama cha soka duniani (FIFA) imeahidi kutoa dola za kimarekani 330,000 (karibu na faranga za Rwanda milioni 277.8) kuelekea mashindano ya (CECAFA) kombe la challenge kwa wanawake yatakayofanyika nchini Rwanda November 3-10 mwaka huu.

Mkurugenzi mtendaji wa kamati ya chama cha soka cha Rwanda Felicite Rwemalika, baada ya mkutano uliofanyika mjini Nairobi mwezi uliopita, bodi ya CECAFA ilichagua Rwanda kuwa mwenyeji wa mashindano hayo ambapo Burundi itaandaa mashindano hayo kwa wenye umri chini ya miaka 17 mwakani. Mashindano hayo yatakutanisha timu kutoka Burundi, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Somalia, Sudan Kusini, Sudan, Tanzania, Uganda na Zanzibar.