Update:

Dereva wa Mbunge shambuliwa kwa shoka na watu wasio julikanaSuezi Dan Maradufu (45), dereva wa Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche ameshambuliwa na watu wasiofahamika usiku wa kuamkia leo na kumjeruhi usoni.

Akiwa amelazwa katika hospitali ya Mji wa Tarime, Maradufu amesema jana Alhamisi saa mbili usiku akitoka nyumbani kwake kwenda kwa mbunge alivamiwa na watu wawili waliomjeruhi kwenye paji la uso.

Maradufu amesema alikuwa akienda kwa Heche ili wasafiri kwenda Nairobi nchini Kenya kumwona Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu aliyelazwa jijini humo baada ya kushambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi nyumbani kwake Area D, mjini Dodoma.

Dereva huyo amesema baada ya kuvamiwa na watu hao, walimpiga kwa shoka kwenye paji la uso na walipora begi lake la nguo. Mrimi Zabron ambaye ni katibu wa mbunge Heche anayemuuguza dereva huyo amesema alifikishwa hospitali saa nane usiku.

Amesema kwa usaidizi wa ndugu wa Heche alifikishwa hospitali na ameshonwa nyuzi sita kwenye jeraha. Zabron amesema safari ya Heche iliyokuwa ifanyike jana saa nne usiku, imefanyika leo asubuhi. Amesema mbunge huyo amesafiri na kaka yake ambaye ni Katibu wa Chadema Mkoa wa Mara, Chacha Heche.

No comments