Update:

Wanariadha waitoa Tanzania kimasomaso kwenye riadha ya Uganda FEASSA
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harisson Mwakyembe amewapongeza wanariadha waliyoshiriki mashindano ya Shirikisho la Michezo Afrika Mashariki FEASSA yaliyofanyika nchini Uganda na kufanikiwa kurudi na Medali. Wanariadha hao ambao ni vijana wadogo wameshiriki katika michezo zaidi ya mitano huku wakikimbia katika mbio za mita 100, 200 na 400.

Katika mbio zote hizo za mita 100, 200 na 400 wameshika nafasi ya tatu na hivyo kuitoa Tanzania kimasomaso miongoni mwa mataifa sita yaliyoshiriki kwa kushika nafasi ya tatu. Akizungumza na wanariadha hao Wazir Mwakyembe amewataka kujituma zaidi ili kuwa mabingwa wa dunia siku zijazo na kuiwakilisha taifa.

No comments