Update:

Wamarekani wamzima Usain Bolt mjini London

Baada ya Usain Bolt kutangaza kwamba anakimbia kwa mara ya mwiso baadhi ya wafuatiliaji wa riadha walisema ni uamuzi mzuri kwani Bolt kwani anaonekana kuanza kupungua kasi.Suala hilo limeanza kuthibitika baada ya Wamarekani wawili Justin Gatlin na Christian Coleman kumshinda Mjamaica huyo katika mbio zamita 100 zilizofanyika hii leo katika jiji la London.

Galtin alikuwa na wakati mgumu sana katika mbio hizo kutokana na mashabiki kumzomea kutokana na kesi yake ya kutumia dawa za kusisimua misuli iliyomfanya kufungiwa mara mbili.

Lakini Galtin alikomaa na kuibuka kidedea akibeba medali ya dhahabu, Bolt hakufanikiwa hata kushika nafasi ya pili kwani nafasi hiyo ilienda kwa Mmarekani Chrstian Coleman na Bolt akachukua ya tatu.Usain Bolt hadi sasa ameshinda medali kubwa za dhahabu 19 huku kati ya hizo nane zikitoka katika michuano ya Olympic ma zingine kumi na moja zilizobaki akishinda kwenye michuano ya World Championship.

No comments