Update:

Wallace Karia rais wa TFFMwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi mkuu wa TFF Revocatus Kuuli amemtangaza Wallace Karia kuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kufuatia uchaguzi wa shirikisho hilo uliofanyika jana Makao Makuu ya Tanzania Dodoma.

Wallace Karia aliibuka mshindi wa nafasi ya Urais wa shirikisho hilo huku nafasi ya Makamu ya Rais ikichukuliwa na Michael Wambura,.


Kwa matokeo hayo Wallice Karia anakuwa mrithi wa aliyekuwa Rais wa shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Jamal Malinzi


Baada ya kutangazwa washindi viongozi hao waliweza kula kiapo mbele ya wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi, na baada ya hapo Rais mpya wa shirikisho la mpira wa miguu (TFF) Wallace Karia aliwashukuru wajumbe na watanzania kIujumla na kusema kuwa furaha aliyonayo iende kuwa furaha ya kazi kwa kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya soka la Tanzania.


Hata hivyo Wallace alisema katika uongozi wake uwazi na uwajibikaji ndiyo nguzo kuu na kusema hivi sasa ubabaishaji katika mpira wa miguu sasa umekwisha, ubabaishaji wa soka sasa ni mwisho.