Update:

Walimu 15 wafukuzwa kazi

Walimu 15 katika wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma wamefukuzwa kazi baada ya kubainika kuwa ni watoro kazini. Tume ya Utumishi na Ajira ya Walimu (TSC0 wilayani humo imefikia uamuzi huo baada ya kushughulikia mashtaka dhidi ya watumishi hao yaliyowasilishwa kwao. Katibu wa TSC Wilaya ya Chamwino, Khalid Shaaban amesema uamuzi huo una gharama, lakini hakuna namna nyingine zaidi kufanya hivyo ili kuchochea uwepo wa nidhamu kwa walimu.