Update:

WALANGUZI WA MAZAO YA WAKULIMA KUDHIBITIWA

Siku moja tangu  Waziri wa TAMISEMI George Simbachawene asema kuwa serikali itadhibiti walanguzi wa mazao ya wakulima; baadhi ya wakulima wamesema kuwa hilo litakuwa jambo jema .

Wakizungumza jana mkoani hapa wamesema kuwa ulanguzi na kutokuwepo kwa uhakika wa masoko kunasababisha kuzorota kwa maendeleo ya kilimo na Wafugaji kukosa mapato stahiki yanayotokana na juhudi zao katika kilimo na ufugaji.

Jana , Akizungumza katika Ufunguzi wa Sherehe za ufunguzi wa 24 ya maonyesho ya Wakulima na wafugaji Nane Kanda ya Kaskazini, Waziri Chawene alisema kuwa  tayari serikali imeanza kutia mkazo katika mazao ili kuleta tija.


Waziri Chawene amewataka walanguzi kuacha mara moja kabla serikali haijawachukulia hatua kwani wanaathiri maendeleo ya kilimo kuanzia kwenye pembejeo hadi kwenye mazao.

No comments