Update:

Wadau wa kandanda Tanzania wamtaka Karia aanze na soka la vijana
Wadau wa soka nchini Tanzania wamemtaka rais mpya wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia kuelekeza nguvu katika soka la vijana ili kuwa na timu nzuri ya Taifa yenye ushindani kimataifa.

Wakizungumza baada ya kuchaguliwa kwa Karia, wadau hao walisema Tanzania bado haijawa vizuri kwenye mashindano ya kimataifa na hilo linasababishwa na kutojiandaa kuanzia ngazi za chini.

Walisema kuwa kutokana na hali hiyo, rais mpya wa TFF anapaswa kuanza na mkakati wa kusaidia kukuza vipaji vya vijana kwa manufaa ya Taifa kwani bila vijana na kutegemea wachezaji wakubwa itakuwa kazi bure.