Update:

Uamisho wa wachezaji barani ulaya


Mshambuliaji wa Brazil Neymar Junior bado anapania kuondoka klabu ya Barcelona na kujiunga na Paris Saint Germain ya Ufaranza. Duru zinaarifu kuwa japo Barcelona inasisitiza kuwa mchezaji huyo hawezikuruhusiwa kugura klabu hiyo, Neymar amewaambia wakaribu wake kuwa anataka kukuhama klabu hiyo ya Uispania hili kujitoa kutoka kivuli cha Messi na kutimiza ndoto yake kuwa mchezaji bora duniani

Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa, 28, hatajiunga na kikosi cha kwanza kwa ajili ya kuanza mazoezi siku ya Jumanne huku akiendelea kufuatilia uhamisho wake kuondoka Stamford Bridge.

Meneja wa Juventus Massimiliano Allegri ameiambia Chelsea kuwa hawatamuuza beki wa kushoto Alex Sandro, 26.

Meneja wa Chelsea Antonio Conte anataka kumsajili kiungo wa Leicester City Danny Drinkwater, 27, baada ya Nemanja Matic kujiunga na Man Utd.

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp huenda akaamua kumfuatilia kiungo wa Bayern Munich Renato Sanches, 19, iwapo Philippe Coutinho, 25, ataondoka kwenda Barcelona.

No comments