Update:

Tottenham yamsajili beki Davinson Sanchez kutoka AjaxTottenham imekamilisha usajili wa beki Davinson Sanchez kutoka Ajax kwa kitita cha pauni milioni 42 kwa mkataba wa miaka 6. Beki huyo mwenye umri wa miaka 21 raia wa Colombia, amekubali mkataba wa miaka 6 akisubiri cheti cha kumruhusu kufanya kazi nchini humo.

Rekodi ya Spurs hapo awali ilikuwa pauni milioni 30 kwa kiungo wa kati wa Ufaransa Moussa Sissoko mwaka 2016. Sanchez atakuwa mchezaji wa pili kusainiwa baada ya mlinda lango Paulo Gazzaniga kujiunga na klabu hiyo kutoka Southampton siku ya Jumatano.

Alijiunga na Ajax kutoka Atletico Nacional mwezi Juni mwaka jana kwa mkataba wa miaka mitano na kushiriki mechi 32 kwa klabu hiyo.

Pia alicheza katika msimu uliopita wa ligi ya Uropa katika fainali ambapo walishindwa na Manchester United na kutawazwa kuwa mchezaji bora wamwezi Mei

Meneja huyo wa Tottenham Pochettino alisema anataka kuwateuwa wachezaji wengine wanne ifikapo mwisho wa dirisha la uhamisho.